Kituo cha usaidizi

Kama ndio mara ya kwanza kujisajili kupakua APP/Programu utaona kurasa ya kuingia, bofya kitufe cha "Jisajili" Au, Nenda ukurasa wa wasifu na kisha bonyeza kitufe cha 'Jisajili' kisha jaza fomu kikamilifu

  • Ingiza namba sahihi ya simu
  • Utapokea jumbe yenye OTP
  • Jaza fomu na kisha weka OTP uliopokea
  • Kubali Vigezo na Masharti
  • Bofya Sajili

Hapana, kwa sasa Bantu ipo Tanzania tu.

Ni rahisi, kwenye app yako, bofya kitufe cha wasifu, kisha nenda kwenye upendeleo, utaweza kukubali au kukataa aina ya majarida.

Ukiwa umefungua tangazo, Bofya kitufe cha ripoti, weka ujumbe wako kama upo na kisha bofya kitufe cha tuma.

Kuna sababu mbili za kwanini tangazo lako linaweza lisionekane:

  • *Linakaguliwa*, Matangazo yote yatakaguliwa na yataonekana katika matokeo ya utafutaji ndani ya saa chache.
  • *Limekataliwa*, Angalia kisanduku pokezi chako, utapokea taarifa ikiwa tangazo lako imeidhinishwa au kukataliwa kwa sababu fulani

  • Bidhaa na huduma zote lazima zifuate sheria na kanuni zinazotumika za nchi.
  • Hakikisha tangazo lina kichwa cha habari kinachoeleweka
  • Hakikisha unajumuisha maelezo mafupi na ya uwazi, ukiepuka taarifa yoyote isiyo sahihi au ya kupotosha
  • Kila tangazo lazima liwe na picha asili zilipigwa na wewe, Upuka kuchukua picha za mtandaoni.
  • Hakikisha umechagua kundi sahihi la bidhaa au huduma yako
  • Bei za bidhaa zako zinapaswa kuendana na viwango vya sasa vya soko kwa bidhaa zinazofanana.
  • Jitahidi kujibu simu zote unazopigiwa mara moja, au upige simu kwa wateja wako haraka iwezekanavyo.

  • Ingia kwenye akaunti yako.
  • Juu kulia bonyeza kitufe chenye alama ya +
  • Jaza fomu kikamilifu na weka picha au video
  • Bonyeza kitufe cha Tuma
  • Kisha subiri, tangazo lako litakagulia na kupitishwa au kukataliwa ndani ya masaa 24

  • Ingia kwenye akaunti yako
  • Bonyeza nenda kwenye ukurasa wa Wasifu, na ubonyeze 'Matangazo'
  • Bonyeza alama ya X kwenye tangazo unalotaka kulifuta

Hakika, sisi si duka. Bantu hutumika kama soko la mtandao ambapo unaweza kutangaza bidhaa au huduma zako, kununua bidhaa kutoka kwa watu binafsi, kutafuta nafasi za ajira, au kupata huduma unazohitaji. Kila shughuli inayofanywa kwa Bantu inahusisha mwingiliano kati ya watu. Jukumu letu ni kuwezesha miunganisho kati ya watu binafsi.

Ndio, Bantu ina mtandao wa maDeliva wa Boda boda na malori madogo kwa ajili ya usafirishaji, unachotakiwa kufanya ni kuomba huduma ya kuletewa kupitia tangazo husika, Gharama zitatozwa kwa mnunuzi

Ifuatayo ni orodha ya bidhaa na huduma ambazo haziruhusiwi kutangazwa kupitia Bantu

  • Madawa ya kulevya, steroidi, na dawa au dawa zozote zinazohitaji maagizo kutoka kwa mtaalamu wa matibabu aliyeidhinishwa.
  • Silaha, Vitu vya kijeshi/polisi vilivyozuiliwa, Viungo vya binadamu, Nakala haramu/zinazoibiwa
  • Vifaa vya kielektroniki vilivyopigwa marufuku na sheria.
  • Huduma zinazozingatia ngono. Mikopo, shughuli za pesa, Bitcoin.
  • Masoko ya ngazi nyingi, piramidi, na programu za matrix.
  • Bidhaa (bidhaa au huduma) zilizopigwa marufuku kuuzwa na sheria.

Msaada zaidi

Jisikie huru kufikia timu yetu ya usaidizi kwa usaidizi zaidi.

What App Chat

Chati na kituo cha msaada kwa wateja moja kwa moja.

WhatsApp

Tuma barua pepe

Tuandikie maoni, malalamiko au maombi ya nyongeza ya huduma.

support@bantu.tz

Tupigie

Onge kituo cha msaada kwa mteja moja kwa moja.

+255 755 135 201